Silicon Lab

Masharti ya Warranty ya Ukarabati

Muda wa Warranty: Miezi mitatu (3) kuanzia tarehe kifaa kilipokamilika kutengenezwa/kubadilishwa.

Warranty inahusu nini: Warranty inahusu tu sehemu (part) iliyobadilishwa au kutengenezwa na Silicon Lab. Ikiwa sehemu hiyo hiyo itapata tatizo tena ndani ya miezi 3, tutaifanyia kazi bila malipo ya ziada.

Warranty haihusu: Uharibifu unaosababishwa na matumizi mabaya ya mteja (mfano: kifaa kuanguka, kuloweka maji, kuvunjika kwa nje, kuguswa na fundi mwingine nje ya Silicon Lab baada ya ukarabati). Katika hali hizi, matengenezo mapya yatatozwa gharama.

Uamuzi wa Warranty: Fundi/menejimenti ya Silicon Lab ndiye anayeamua, baada ya uchunguzi, kama tatizo linaloletwa linahusiana na kazi iliyofanyika awali (linalostahili warranty) au ni tatizo jipya/uharibifu wa mteja.

Kwa maswali zaidi kuhusu warranty ya kifaa chako, wasiliana nasi kupitia WhatsApp au tembelea ofisi yetu.

← Rudi kwenye Ombi la Ukarabati

Wasiliana Nasi kwa WhatsApp