Sera ya Faragha (Privacy Policy)
Taarifa Tunazokusanya
Tunapokuhudumia, tunaweza kukusanya taarifa zifuatazo kutoka kwako:
- Jina lako na namba ya simu (kwa ajili ya oda, huduma za ukarabati, na uthibitisho wa akaunti)
- Taarifa za kifaa unachotengeneza (aina ya kifaa, chapa, model, IMEI/serial namba, maelezo ya tatizo)
- Anwani/eneo la delivery unapoagiza bidhaa
- Historia ya oda na ukarabati wako
- Maoni/testimonial unayotuma - yakikubaliwa na admin, yanaonekana hadharani kwenye website pamoja na jina lako
Kwa Nini Tunakusanya Taarifa Hizi
- Kuthibitisha akaunti yako kupitia SMS ya uthibitisho (OTP) - tunatumia huduma ya Beem Africa kutuma code hii
- Kushughulikia oda zako na kukujulisha status ya ukarabati wa kifaa chako
- Kuwasiliana nawe kuhusu kifaa chako kupitia WhatsApp - ujumbe huu unaundwa na kutumwa na wewe mwenyewe unapobonyeza kitufe cha order
- Kuboresha huduma na bidhaa zetu
Nani Anaona Taarifa Zako
Taarifa zako haziuzwi wala kusambazwa kwa makampuni ya tatu kwa madhumuni ya matangazo. Tunatumia huduma zifuatazo za nje kwa uendeshaji wa mfumo pekee:
- Beem Africa - kutuma SMS za uthibitisho (OTP)
- Google - kuonyesha maoni ya Google Reviews na location ya duka kwenye Google Maps
Muda wa Kuhifadhi Taarifa
Tunahifadhi taarifa zako kwa muda unaohitajika kwa uendeshaji wa biashara na kama inavyotakiwa kisheria, mfano rekodi za mauzo na ukarabati.
Usalama wa Taarifa
Namba yako ya simu inathibitishwa kwa OTP badala ya password ili kupunguza hatari ya wizi wa akaunti. Taarifa zote zinahifadhiwa kwenye database iliyolindwa, na akaunti za wafanyakazi wanaoweza kuziona zina ulinzi wa nywila.
Haki Zako
Una haki ya kuomba kuona, kurekebisha, au kufuta taarifa zako tulizonazo. Wasiliana nasi kupitia namba ya simu au WhatsApp iliyopo chini ya website hii.
Mabadiliko ya Sera Hii
Tunaweza kubadilisha sera hii mara kwa mara ili kuendana na huduma zetu. Mabadiliko yoyote yataonekana kwenye ukurasa huu.